NSSF kirefu chake ni National Social Security Fund. Hii ni taasisi ambayo inahusika na kukusanya kiasi cha mishahara ya wafanyakazi, kuwekeza kwenye miradi mbali mbali na kulipa wafanyakazi endapo watastaafu kazi au kusimamishwa kazi ili kuwasaidia kipindi hawatokua na ajira.

Kama umesajiliwa na mfuko wa NSSF unaweza tumia njia ifuatayo kujua salio lako:

Kutumia simu yako andika neno NSSF balance mbele yake andika namba yako ya NSSF af tuma ujumbe kwenda namba 15200.

Au endapo unataka kujua statement ya NSSF yako andika neno NSSF statement kufuatiwa na namba yako ya NSSF na meseji hii tuma kwenda namba 15200.

Taarifa hii utakayo pata kwenye simu yako sio lazima iwe ya uhakika. Kuna mda mwengine inakua tofauti kidogo kutokana na mtandao wao wenyewe. Ingaweje hii taarifa utakayo ipata itakua ni sawa au karibu na kiasi kile ulichonacho. Kwa taarifa za uhakika zaidi tembelea ofisi za NSSF karibu na uulize utapata maelezo ya uhakika.

Address za NSSF Dar es salaam