Tanzania kwa sasa imeamua kuama mfumo wa kizamani wa kulipia cash wakati wa parking na kuamia kulipisha kidigitali kwa njia ya simu. Hii yote imeletwa kutokana na changamoto kubwa iliokua ikisababisha pesa nyingi ya serikali kutofika serikalini.

TARURA ni Taasisi ya serikali ambayo inahusika na ukusanyaji wa hizi fedha za parking barabarani.

Nakala hii itakuelekeza jinsi ya kuangalia chombo chako cha usafiri kinadaiwa bei gani na namna ya kulipa deni hili ili kuepukana na faini.

Jinsi ya kuangalia deni la parking

  1. Bonyeza *152*00#
  2. Chagua namba 4 (Nishati, madini na usafiri)
  3. Baada ya hapo chagua namba 2 (Tarura)
  4. Kisha chagua namba 2 (Termis/angalia deni)
  5. Ingiza namba ya usajiri wa chombo cha usafiri mf. T544 AZZ
  6. Utapokea ujumbe mfupi wenye deni lako na kumbukumbu namba ya malipo.

Jinsi ya kulipia car parking

  1. Bonyeza *152*00#
  2. Chagua namba 4 (Nishati, madini na usafiri)
  3. Baada ya hapo chagua namba 2 (Tarura)
  4. Kisha chagua namba 1(Lipia Maegesho)