Nakala hii itakuelekeza namna ya kupata namba ya nida na kuangalia kwa njia ya mtandao endapo utakua umesahau au kujua kama imeshatoka tayari baada ya usajili.

Namba ya nida ni muhimu sana katika nchi ya Tanzania. Endapo wewe ni mwananchi Tanzania namba ya nida imekua kama lazima uwe nayo ili uweze pata huduma mbali mbali.

Kuanzia mwaka 2021, huwezi kusajili kupata namba ya simu bila kuwa na namba ya nida, huwezi fungua account bank bila kuwa na namba ya kitambulisho cha nida, kiufupi huduma zote za kiserikali na zengine nyingi huwezi pata bila kuwa na kitambulisho cha nida

Hivyo basi mtu yeyote ni muhimu kuwa na namba ya nida kama unaishi Tanzania.

Kama umesahau namba yako ya nida unaweza pata kwa kujaza taarifa zako chache kupitia link hii hapa chini

https://services.nida.go.tz/nidportal/get_nin.aspx

Jinsi ya kupata namba ya nida

Namba ya kitambulisho ya NIDA huwezi pata online ni lazima kutembelea ofisi husika katika mkoa unaoishi ndio ufanyiwe usajili. Katika ofisi hizo wanakawaida ya kuhoji maswali ya mahali ulipo zaliwa, majina ya wazazi wako, kabila, umesoma wapi na mengine mengi kuthibisha kama wewe ni mtanzania. Baada ya hapo utapewa siku ya kwenda kuchukua namba yako kama ukibahatika unaweza pewa na kitambulisho kabisa.

https://www.dawazetu.co.tz